- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADIWANI WENGINE WA UPINZANI WATIMKIA CCM
Bukoba: Madiwani wawili kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na mmoja kutoka chama cha NCCR-Mageuzi manispaa ya Bukoba wamejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM, Akiwemo meya wa zamani wa manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.
Dk Aman aliyekuwa diwani wa Kagondo Agosti 20, 2015 alihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi na kuwania udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015. Mbali na Dk Aman, mwingine ni aliyekuwa diwani wa Hamugembe (Chadema), Muhaji Kachwamba. Wote wameshakabidhi barua za kujivua nyadhifa zao katika ofisi za CCM Mkoa wa Kagera tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali.
Akitaja sababu za kurejea CCM, Dk Aman amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli. Amesema CCM ni sehemu sahihi ambayo anaweza kumsaidia Rais Magufuli kutekeleza ilani ya chama hicho tawala, kubainisha kuwa ameondoka NCCR na waliokuwa wakimuunga mkono. Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Bukoba, Ioas Muganyizi amesema milango bado ipo wazi kwa wanachama wengine wanaotaka kujiunga na chama hicho.
Kumekuwa na mfululizo wa wanasiasa wa wabunge na madiwani kutoka vyama vya upinzani CUF na Chadema wametangaza kujiengua katika vyama vyao ikiwemo kujiuzulu nafasi zao za uongozi na kutimkia CCM.
Naibu meya wa manispaa ya ilala, na diwani wa vingunguti Omari kumbilamoto amejiuzulu nafasi ya udiwani na umeya lakini pia amejivua uanachama wa CUF.
Mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga Laizer amejiuzulu na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Kabla ya kalanga kujiuzulu alikuwa ni mwanasiasa wa upinzani, Mwita Waitara alitangaza kujiengua katika chama kikuu cha upinzani cha chadema na kujiunga na Chama tawala, CCM.
Waitara aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga lililopo Dar es salaam alikishutumu chama cha Chadema, kuwa hakina demokrasia pia kutokuwa na maelewano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Ikumbukwe kuwa wabunge hawa wote yaani Waitara na Kalanga waliwahi kuitumikia CCM, ambapo Waitara aliitumikia CCM mwaka 1998 mpaka mwaka 2008 wakati Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM.
Hata hivyo baada ya kujiengua baadhi yao wamepata neema ya kuteuliwa na rais katika baadhi ya nafasi za uongozi. Wiki iliyopita Rais Magufuli alimteua David Kafulila kuwa katibu tawala wa mkoa wa Songwe.
Awali Kafulila alikuwa mbunge wa chama cha upinzani NCCR-Mageuzi.
Pia alimteua Moses Machali kuwa mkuu wa wilaya ya Nanyumbu. Kabla ya uteuzi huo Machali aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu mjini kupitia NCCR-Mageuuzi ambapo baadaye alihamia ACT-Wazalendo kisha kwenda CCM.
Mwanasiasa mwingine aliyepata fursa hiyo ya kuteuliwa na Rais ni Patrobas Katambi ambaye amekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma, Kabla ya hapo Katambi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chadema.