- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADHARA YA KUNUNG'UNIKA.
Kunung’unika kuliwafanya wana wa Israeli kushindwa kufika katika nchi ya ahadi.
Katika kitabu cha hesabu tunaona jinsi ambavyo walilalamika baada ya wale wapelelezi kuleta habari za nchi ya ahadi. Hesabu 13:31-33, 14:1-4. Katika habari hii tunajifunza mambo yafuatayo:
i) Unaponung’unika unapuuza uwezo wa Mungu
Wana wa Israeli walisahau na kupuuza uwezo wa Mungu aliyewatoa Misri utumwani na kuwavusha katika bahari ya Shamu na kuwapigania katika safari yao na kuona kuwa lililo mbele yao haliwezi na kuishia kunung’unika na kulalamika.
ii) Kungu’unika huchochewa na taarifa isiyo sahihi
Uchochezi, uongo, majungu n.k huchochea kunung’unika kutokana na kuwa huleta habari ambazo sio sahihi zenye lengo la kuharibu na kuangamiza. Kuna watu wanapenda kusikia habari mbaya za watu wengine au jambo Fulani ili wapate kitu cha kulalamika na kulaumu.
iii) Mtu anayelalamika ni rahisi kufikia maamuzi ambayo si sahihi
Wana wa Israeli walimlaumu Mungu kwa hali waliyoisikia kuhusu nchi ya kanaani na hata kufikia hatua ya kupanga kurudi Misri.
iv) Katika hali ya kulalamika, ni rahisi kufanya mambo mabaya bila kufikiria.
Wana wa Israeli katika kulalamika na kunung’unika kwao walitaka kuwapiga mawe wale walioleta taarifa nzuri kuhusu kanaan. 14:10. Kunung’unika kunakufanya ushindwe kufikiri kwa makini na kuona uhalisia wa jambo husika.
v) Kunung’unika huzidi katika mazingira ya hofu
Hofu ya wana wa Israeli iliwapelekea kunung’unika, japo Joshua na caleb waliwatoa hofu kwamba wasiogope wao bado walijawa na haofu hali iliyowapelekea kuzidi kunung;unika hasa kwa kutokujua nini kitatokea baada ya kusahau kabisa ukuu wa Mungu.
vi) Kunung’unika kukiachwa kuendelea hupelekea uasi
Wana wa Israeli walikuwa tayari kuchagua viongozi wengine na kuasi mbele za Mungu na kurudi Misri. Hii ilitokana na kunungu’unika kwao hadi wakaona kuwa wao ndio wanaojua zaidi ya Mungu.
vii) Mwisho wa kunung’unika ni kuwa mtu asiyeridhishwa na chochote
Unapoendelea kunung’unika unazidi kuona kila kitu ni kibaya na hakifai. Wana wa Israeli walipewa kila kitu na Mungu na bado hawakuridhika kwa sababu ya tabia ya kunung’unika.
Sababu ya kunung’unika kwao hawakuona upendo wa Mungu, wala ukuu wake wala uzuri wa nchi ya ahadi wao waliona mabaya tu.
Kunung’unika ni jambo linalotutoa kwenye uwepo wa Mungu. Mtu anayenung’unika hana imani kwa Mungu na nguvu yake. Ni hali ya kutokuamii kuwa Mungu anaweza akatumia mambo magumu uanayotokea katika maisha yetu kwa ajili ya kutupatia mema aliyoyakusudia.
Ili kuepuka kunung’unika na kuweza kutatua tatizo linaloweza kufanya ulalamike na kunung’unika unahitajika:
1.Kuomba
Kwa maombi tunayapeleka matatizo yetu kwa Mungu, na kumsubiri aweze kutuongoza katika njia sahihi.
2. Malalamiko yako yapeleke kwa wahusika
Unapozungumza tatizo Fulani na mtu asiyehusika unakuwa unachangia manung’uniko na kulizidisha tatizo hilo. Ongea na wahusika kwa utaratibu na busara, uwe tayari kusikia maoni yake na ufafanuzi na pia uwe tayari kubadili msimamo wako pale utakapopata taarifa sahihi.
3. Waeleze wengine wanaonung’unika nini cha kufanya
Usipende kuwa sehemu ya manung’uniko ya watu wengine wala kuwachochea kuendelea kulalamika. Waonyeshe nani wamwendee ili kupata majibu ya maswali yao.