Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:37 pm

NEWS: MADHARA YA CHADEMA KUJIONDOA KWENYE CHAGUZI ZIJAZO

Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema jana kimetangaza uamuzi wa kutoshiriki chaguzi zozote ndogo zinazoandaliwa na tume ya Uchaguzi Tanzania NEC.

Uamuzi wa Chama hicho umekuja siku chache baada ya kushindwa na Chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM katika chaguzi mdogo ziliomalizika wiki iliyopita katika majimbo ya Ukonga Mkoani Dar es Salaam na Monduli Mkoani Arusha sanjari na kata kadhaa nchini humo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman mbowe ameambiwa wanahabari Jijini Dar es Salaam kuwa chama chake kimechukua uamuzi huo kutokana na uvunjifu wa sheria na mifumo ya uchaguzi inayoendelea nchini humo.

"Kwa sasa tunakwenda kufanya mabadiliko ndani ya chama, tunakwenda kujijenga, hatuwezi kushiriki wakati tunaonewa na sheria hazifuatwi.Kwa sasa tunarudi nyuma,"ameeleza Mbowe, mbunge wa kuchaguliwa katika Jimbo la uchaguzi la Hai, Mkoani Kilimanjaro.

"Ninafahamu kila anayerubuniwa kuunga mkono juhudi anasema kikwazo ni Mimi Mwenyekiti lakini ni mpango wa CCM kutaka kudhoofisha Chama chetu, ningekuwa dhaifu CCM wangefurahi sana lakini niwaahidi viongozi na wanachama sitokuja kupiga magoti kwaajili ya CCM" Freeman Mbowe.

Malalamiko ya Chadema yanakuja wakati ambao Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania ikisema chaguzi ndogo zilizomalizika hivi karibuni ziliendeshwa kikamilifu kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uchaguzi.

Tanzania itashuhudia uchaguzi mwingine mdogo katika Jimbo la Liwale, Kusini mwa nchi hiyo baada ya aliyekuwa mbunge wake Mohammed Kuchauka kujiuzulu na kujiunga na CCM ambayo imemteua kuwania ubunge kwenye jimbo hilo.

Aidha kata nyingine 37 zinatarajiwa kufanya chaguzi ndogo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya waliokuwa madiwani wake kujiuzulu kwa madai ya kuunga mkono serikali ya rais John Magufuli.

Nini Athari za chama hicho kujiengua.

Wakati chadema wakitangaza uwamuzi wa kutoshirini katika chaguzi za marudio zijazo, baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanaona kama ni sehemu ya kukifanya chama tawala CCM kukipa Tiketi Rasmi ya kuondoa upinzani nchini.

Muakilishi Media imepiga stori na Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu cha ARDHI jiji Dar es salaam kwa sharti la kutotajwa jina alisema kuwa uwongozi uliopo sasa hautaki siasa zenye upinzani kwahiyo kama chama kikuu cha upinzani kinainua mikono ya kutoshiriki katika chaguzi za marudio zijazo, maana yake chama cha CCM kinakuwa kimeshinda kampeni yake ya kutokuwa na upinzani nchini "na uchaguzi utakuwa halali na utaonekana wa Demokrasia kwa sababu vipo vyama vingine vingine vya upinzani ambavyo vinaonekana kama wakala kwa chama tawala ambavyo vitashiriki chaguzi hizo, kwamaana hiyo chadema watakuwa wamepoteza bure" alisema Mkufunzi huyo

Amewahi kunukuliwa na vyombo vya habari katibu wa itikadi na uenezi wa CCM hamphry polepole akijinasibu na kuahidi watu kuwa ifikapo 2020 kwenye uchaguzi mkuu hakutakuwepo na upinzani nchini na amekuwa akiwahakikishia na kuaambia baadhi ya wabunge machachali wa upinzani nchini akiwemo mbunge wa kigoma Mjini Zitto kabwe kuwa hawatarudi bungeni baada ya uchaguzi wa 2020

Katika hatua nyingine Mbowe amesema hana mpango wa kujizulu wadhifa wake wa uenyekiti katika chama hicho.