- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADEREVA WA BODABODA WAKATISHA NDOTO ZA WANAFUNZI KWA KUWAPA MIMBA.
DODOMA: Zaidi wasichana ya 250 wa shule za msingi na sekondari katika kata nne wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma wameacha masomo kutokana na mimba za utotoni sababu kubwa inayosababisha kuwapo kwa tatizo hilo ni umbali kutoka nyumbani wanakoishi hadi shuleni na kukutana na vishawishi pamoja na umasikini wa kaya.
Takwimu ambazo zimetolewa na wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, mkoa wa Dodoma unashika nafasi ya tatu kwa tatizo la mimba za utotoni huku wilaya ya mpwapwa ikitajwa kinara mkoani humo.
Evance Lwamuhuru ni mtafiti kutoka shurika lisilo la kiserikali la utu wa mtoto amesema kuwa utafiti umebaini katika kipindi cha miaka mitano idadi hiyo ya wasichana wameacha masomo kutokana na tatizo kubwa kuchangiwa na wazazi kuwaficha watoto na wahusika wa ukatili huo kwa maslahi yao binafsi.
Naye afisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Antony Mlabile, anakiri tatizo hilo ni kubwa na jitihada mbalimbali zikiendelea kufanyika ili kukabiliana nalo lakini zinakabiliwa na usiri uliopo miongoni mwa jamii.
Kwa upande wake, Mwalimu Agness Anthony wa shule ya msingi Ilolo wilayani humo anasema mbali na vishawishi na ugumu wa maisha lakini pia matumizi mabaya ya teknolojia na malezi mabovu ni sababu kubwa ya wanafunzi kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa na umri mdogo.
Baadhi ya mabinti ambao ni maadhura wa mimba za utotoni wanasema hali ngumu ya maisha kwenye familia inachangia kwa kiasi kikubwa kupata tatizo hilo pamoja na ushawishi kutoka kwenye makundi yasiyofaa.
Kundi la Bodaboda ni miongoni mwa makundi yanayotajwa kuleta vishawishi na kusababisha watoto wa kike kukatisha masomo ambapo Abubakary Fikirini ambaye ni dereva wa bodaboda anakiri kuwepo kwa changamoto hiyo.
Jamii inapaswa kukemea na kudhibiti tatizo la mimba za utotoni ili kumwezesha mtoto wa kike kufikia ndoto zake