- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MADAKTARI WAGOMA WAKIDAI SHINIKIZO LA MSHAHARA UGANDA
Madaktari Uganda wafanya mgomo wakidai nyongeza ya mishahara
Madaktari wa Uganda wameanza mgomo wa nchi nzima baada ya serikali kushindwa kutekeleza matakwa yao kuhusu nyongeza ya mshahara na kuboresha mazingira ya kazi katika hospitali za umma.
Madaktari hao wanaoongozwa na Shirikisho la Matibabu la Uganda UMA wameanza mgomo baada ya kukataa wito wa kusimamisha mgomo uliotolewa na Waziri Mkuu Bw. Ruhakana Rugunda, na maofisa wa wizara ya afya katika mkutano wa pande mbili uliofanyika jana huko Kampala.
Mwenyekiti wa UMA Bw. Ekwaro Obuku amesema, mgomo huo utaendelea hadi serikali itakapokidhi mahitaji yao kuhusu kuboresha malipo, upungufu wa dawa na vifaa ili waweze kufanya kazi vizuri.
Juhudi za Waziri wa Afya Sarah Opendi kuwashawiswhi madaktari kusitisha mgomo huo wakati serikali ikishughulikia madai yao ziligonga ukuta.
Waziri Mkuu Dkt Ruhakana Rugunda aliitwa katika mkutano huo lakini akawa na wakati mgumu kuwahutubia madaktari na kuondoka kwa hasira.
Naibu mkuu wa muungano wa madaktari nchini Uganda Profesa Pauline Byakika, ameeleza kwamba mgomo huo hauwezi kuepukika.
Kati ya matakwa ya madaktari ni kuongezwa mishahra na marupurupu, kupewa nyumba na usafiri. Iwapo serikali itasikiliza matakwa ya madaktari basi watapata mshahara wa Shs milioni 8.5 kwa mwezi badala ya mshahara wa sasa wa Shs 1.1 million za Uganda ambao ni takribani dola 300.
Madaktari hao wanajiunga na wasimamizi wa mashtaka ambao mgomo wao unaingia mwezi wa pili sasa.
Muungano wa wanasheria nchini Uganda, umekuwa ukisaidia katika mazungumzo kati ya serikali na wasimamizi wa mashtaka kujaribu kutatua mgomo ambao sasa umeingia mwezi wa pili, wasimamizi wa mashtaka wakitaka nyongeza ya mishahara na mazingira salama ya kazi.