- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MABULA AWATAKA WALIOVAMIA MAENEO WAONDOKE HARAKA IWEZEKANAVYO.
DODOMA: Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula ametoa rai kwa taasisi za serikali kuhakikisha zinapima na kumilikishwa maeneo yao ili kuwa na milki salama kwa kuwa ulinzi wa ardhi wanayoimilki ni jukumu la taasisi husika.
Akijibu maswali ya mbunge wa viti maalum Angelina Malembeka aliyetaka kujua(a) ’’je serikali itakamilisha upimaji wa maeneo hayo’’ (b) je, kutokana na ukubwa wa gharama za upimaji kwanini zoezi la upimaji lisitolewe bure kwa taasisi za umma kupitia halmashauri zao’.
Mabula Amesema maeneo ya shule, soko, zahanati,vituo vya afya, hospital, vyuo,ofisi za serikali, vituo vya polisi, Mahakam, maeneo ya majeshi, hifadhi za misitu na wanyama na maeneo ya majeshi, hifadhi za misitu na wanyama na maeneo ya m,akumbusho hutengwa maalumu kwa ajili ya matumizi ya umma na shughuli mbalimbali za serikali.
Aidha amesema pamoja na utaratibu umekuwa ukitumika kwa nia njema , umetoa mwanya kwawananchiwenye nia ya ovu kuyavami, kuayamega na kuyaendelea ya serikali kinyume na utaratibu.
Hata Amesema ili kuhakikisha changamoto ya uvamizi wa maeneo ya ummaunakomeshwaserikali kupitia wizara yangu iliagiza kuwa maeneo yote ya umma yapimwe na yamilikishwe kwa taasisi husika kupitia barua yenye kumb.Na. AB225/30/305/01 ya tarehe 7 septemba , 2016 .
Mbali na hayo ametoa rai kwa wakuu wa taasisi za umma kuhakikisha wanamilikisha zoezi hilo mapema na kwa maeneo yaliyovamiwa ni vema wavamizi waondoke kwa hiari yao wasisubiri mkono wa sheria uwakumbe.