Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 6:28 am

NEWS: MAALIM SEIF AMTAKA RAIS MAGUFULI KUKAA KWENYE MEZA YA MAZUNGUMZO

ZANZIBAR: Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif sharif Hamad amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli kuketi nae meza moja ili kujadili mustakabali wa masuala yahusiayo Zanzibar.

Akiongea kupitia Ukurasa wake wa Twitter leo May 24 Seif amesema kuwa kipindi cha Uchaguzi kabla ya ZEC Kutangaza matokeo Wakati wameanza kukutana ili kujadiliana, mustakabali wa Zanzibar upande wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) chini ya Mwenyekiti wake Jecha SalimJecha waliwazunguka wakatangaza uchaguzi mwingine mpya huku kwenye katiba ya Zanzibar kukiwa hakuna kipengele cha marudio ya uchaguzi.

''Wakati tumeanza kukutana ili kujadiliana, wenzetu wakatuzunguka wakajitangazia uchaguzi mwingine mpya bila kujali kuwa Katiba ya Zanzibar haina kipengele kinachoruhusu kurudiwa kwa uchaguzi'' amesema Seif

Shein amesema kuwa kwa sababu yeye ni mtu asiyependa kabisa vurugu, baada ya hatua ile ya ZEC alimwandikia barua Dk. Shein kumuomba wakutane, "akanijibu tukutane na wajumbe wengine, nikakubali, tukakutana"

Tokeo la picha la maalim seif na rais magufuli

Seif ameendelea kusisitiza maridhiano waliyofikia kati yake na Mtangulizi wa Rais chein 2010 Aman Karume ambayo yalifanya Zanzibar kutia hayakufanyika kwa matashi yake wala Karume Bali yalikuwa ya Wazanzibari kwa Ujumla wake.

''Maridhiano ya mwaka 2010 hayakuwa ya Maalim Seif na Karume, yalikuwa ya Wazanzibari wote na ndiyo maana yalithibitishwa na Baraza la Wawakilishi na Wananchi wote kupitia kura ya maoni'' aliandika Shein