- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAALIM SEIF AKOSOA VIKALI MAAMUZI YA SEREKALI KATIKA MKATABA WA GESI
Zanzibar: Taarifa kutoka visiwani Zanzibar zinaripoti kuwa Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekosoa vikali makubaliano yaliyofikiwa katika utiaji saini baina ya Serekali ya Zanzibar na Kampuni ya Ras-Alkhaima dhidi ya uzalishaji wa Mafuta na Gesi asilia visiwani humo, huku akidai kuwa mkataba huo katika mgawanyo umekiuka katiba, sheria za nchi na haukufuta utaratibu unaotakiwa kama nchi.
Akiongea leo Jumapili Novemba 11 na waandishi wa habari Maalim Seif amedai mkataba huo umesainiwa katika mazingira yaliyokosa umakini na utasababisha vizazi vijavyo kuingia kwenye janga kubwa la kutofaidika na rasirimali hiyo endapo itapatikana.
Lakini Oktoba 23, 2018 wakati hafla ya utiaji saini mkataba huo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein alisema mchakato huo umezingatia sheria zote za Zanzibar na si vinginevyo.
"Mwaka 2010 kampuni hiyo ilinunua hisa za leseni ya kampuni ya Antrim kuhusu kitalu cha Zanzibar na Pemba na kurithi mkataba wa mgawanyo wa faida kutoka Antrim.β
"Hii si mara ya kwanza ya kitalu hicho kufanyiwa marekebisho sawa na yaliyotiliwa saini Oktoba 23. Makubaliano hayo yalishaingiwa miaka 22 kilichobadilika ni tarehe na watiaji saini na katarasi za makubaliano," amesema Maalim Seif.
Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amesema mwaka 2016 Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipitisha Sheria ya Mafuta ya Zanzibar ambayo kimaudhui haina na tofauti na Sheria ya Mafuta ya Bunge mwaka 2015