Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:46 pm

NEWS: LUGOLA AWAPINGA MGAMBO WA PAUL MAKONDA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Kangi Lugola imelaani vikali vitendo vya watu kujichukulia sheria mkononi ikiwemo kupiga, kujeruhi na kuuawa.

Akizungumza leo Jumapili Septemba 2, 2018 Waziri Lugola amesema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza. Image result for kangi lugola na waandishi

Ametaja matukio ya walimu kuwaadhibu, kujeruhi na kusababisha vifo vya wanafunzi wao pamoja na mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kuwajeruhi wananchi wanaposimamia suala la usafi kuwa miongoni mwa matukio yasiyokubalika mbele ya macho ya sheria. "Suala la mgambo waliowekwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwapiga na kuwajeruhi wananchi limewaondolea sifa ya kuendelea kuwatumikia wananchi, ni vema halmashauri ikatafuta njia mbadala ya kushughulikia suala hilo la usafi na kudhibiti matukio hayo," amesema Waziri Lugola

Ameagiza halmashauri nchini kuanzisha kitengo cha huduma ya askari polisi chini ya sheria sura ya 322 ili kupunguza matukio ya mgambo ambao baadhi hawajui namna ya kusimamia utekelezaji wa sheria kutumika na hatimaye kukiuka sheria. Akizungumzia adhabu kwa wanafunzi, Waziri Lugola amewataka walimu kutoa adhabu kwa mjibu wa sheria kwa lengo la kuwarekebisha wanafunzi na si kuwakomoa.

Ameuhakikishia umma kuwa Serikali kupitia mamlaka husika itachukua hatua dhidi ya wote waliohusika katika matukio yote ya kujichukulia sheria mkononi. "Mahakama pekee ndicho chombo cha kutoa adhabu kwa mujibu wa Katiba na sheria. Tutawashtaki wote waliohusika bila kujali vyeo, majina wala umaarufu wao kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria," amesema Lugol