- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA ASEMA BADO WANAWATAFUTA WALIOMTEKA MODEWJI
Dar es salaam: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Serikali kupitia Jeshi la Polisi inaendelea kuwatafuta watu wote waliomteka Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Dodoma leo Jumapili Oktoba 28, Waziri Lugola, amesema bado msako unaendelea kuwatafuta wale wote waliomteka mfanyabiashara huyo.
“Niendelee kuwasihi ndugu zangu, mmekuwa mkitaka sana kujua tunaendeleaje kuwatafuta watekaji wa Mo, mimi nimeendelea kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi linashughulika na matukio yote ambayo yametokea na kama kuna matukio yametokea ya mtu kupotea haonekani wote hao kwa ujumla wao tutayashughulikia.
“Wale ambao hatujawapata bado Jeshi la Polisi tunaendelea kuwatafuta hadi yule wa mwisho atakapotiwa mbaroni kwa hiyo ninyi msidhani kwamba hatuwatafuti kila mkiuliza mnaulizia Mo tu tunaomba muwe waangalifu,” amesema.
Kugola pia amesema hatua hiyo italeta dhana kwamba watu wa kawaida wanapopata matatizo hawana thamani au pengine serikali haiwatafuti wale waliofanya uhalifu, na kuongeza kuwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hawezi kuacha hilo likaendelea
Mfanyabiashara huyo alitekwa Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam na kupatikana Oktoba 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini humo.