- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA APIGA MARUFUKU TRAFIKI ASIE NA JEZI KUKAMATA BODABODA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi nchini kukamata waendesha pikipiki (bodaboda) wakiwa hawana sare za jeshi.
Kauli hiyo ameitoa Jana January 3 wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru maarufu Mayunga mjini Bukoba mkoani Kagera jana, Lugola alisema polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.
“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola. Pia aliwataka waendesha bodaboda mjini Bukoba na Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa koa ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa"
Pia akawataka Askari kuacha tabia ya kuoa faini nyingi kwa Gari ambalo ni Bovu" Ukikamatwa na Trafiki akakuambia bodi ya gari bovu,tairi kipara,maji ya wepa hayatoki,taa za breki haziwaki, hapo kosa ni MOJA tu, gari ni bovu na faini ni TZS30,000, na si sahih kuwa kila tatizo la gari ni kosa linalojitegemea,linalostahili kutozwa faini tofauti tofauti" LUGOLA