- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA AAHIDI KUMTOA TUMBO MWANASIASA MCHOCHEZI
Dodoma: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa yupo radhi kumtoa tumbo mwanasiasa au mtu yeyote atakaye Fanya siasa za uchochezi hapa nchini.
“Siko tayari kutumbuliwa ila niko tayari kuwatoa matumbo wote watakaokuwa wanajihusisha na uchochezi kabla tumbo langu halijatumbuliwa na mheshimiwa Rais,” alisema Lugola alipozungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa.
Lugola alivionya vikali vyama vya siasa ambavyo vinavyo shiriki Katika chaguzi
“Navionya vyama vyote vya siasa, mtu yoyote wa chama chochote cha siasa atakayeonekana akitumia kinywa chake kutoa matamko ambayo ni ya uchochezi ajue kwamba hayuko salama tutamkamata hata kama ni mgombea yuko katika jukwaa,” alisema
Kauli hiyo ya kuvionya vyama vya siasa imekuja wakati vyama hivyo vipo kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa madiwani na ubunge, utakaofanyika Agosti 12.
Lugola alisema mgombea atakayetoa matamshi ya uchochezi atakamatwa na huenda akakosa haki ya kuendelea na uchaguzi.
“Hii ni kwa sababu haturuhusu mtu atoe matamshi ya kutukana viongozi, matamshi ya uchochezi atakuwa amepoteza nafasi yake ya kuomba kura labda bahati yake kama wananchi wanamtaka kumchagua bila kuendelea na kampeni,” alisema.
Alionya kuwa asisikie mtu yoyote anatoa kauli ya uchochezi atapambana naye na kwamba yeye aliapishwa na Rais John Magufuli ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na amani, usalama na utulivu.
Lugola alisema pia Rais Magufuli wakati anaapishwa kushika uongozi wa nchi, aliahidi kuendelea kudumisha uhuru, amani, usalama na kuwalinda Watanzania.
Alisema hayuko tayari kuwafumbia macho wanaofanya uchochezi kwa kuwa huko itakuwa ni kumuangusha Rais Magufuli.