- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LOWASSA AIJIA JUU CCM, ASEMA HAWEZI KURUDI
Meru: Aliyekuwa Mgombea Urais mwaka 2005 kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa hana mpango wa kurudi CCM, watu wanajaribu kutengeneza ili kuhadaa wananchi, akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za udiwani jana jumanne (21.11.2017) katika Eneo la Makiba wilaya ya Meru Lowassa amekanusha tuhuma hizo zilizozagaa mitandaoni "Leo(Jana) nimeona kwenye mitandao kuna mtu anasema nimemtumia watu wamueleze kwamba nataka kurudi CCM! Siwezi kurudi CCM, hayo ni maneno ya kibuuzi" alisema Lowassa.
Kauli ya Waziri mkuu huyo wa zamani imekuja mara baada ya kuwepo kwa wimbi la wanasiasa mbalimbali kutoka vyama tofauti kuhamia CCM na wengine kuhamia chadema.
Lowassa alihoji juu ya wimbi la wanasiasa hao kuhamia CCM kuwa ni kwa sababu ya kuwepo kwa ubaguzi wa ukanda na akatumia fursa hiyo kuitaka serekali kuacha mara moja tabia ya kuongozi nchi kwa ukabila "Nikajiuliza, hata Patrobas? nikagundua oooohh kumbe nimsukuma .... Ndio maana!. ninaiomba serekali ya CCM iache mara moja kutuongoza kwa ukabila. taifa letu halikujingwa katika misingi hiyo" alisema Lowassa.
Jana chama Tawala cha CCM kupitia mkutano wao mkuu NEC kilipokea wanachama wapya takribani 6 akiwemo Sophia Simba ambaye alinyang'anywa kadi ya uwanachama Miezi kadhaa iliyopita baada ya kuonekana na utovu wa nidhamu mbele ya chama hicho.
Wanasiasa waliotambulishwa CCM Jana kupitia mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Pombe magufuli nipamoja na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa ndg. Patrobas, aliyekuwa mwanasheria na mshauri wa ACT Wazalendo Wakili Albert Msando, aliyekuwa Katibu mkuu kitengo cha mawasiliano ACT Wazalendo Samson Mwigamba , Laurence Masha na Prof. Kitila Mkumbo