- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU KUPELEKWA NJE YA KENYA KUFANYIWA MATIBABU YA VIUNGO.
DODOMA: Wakili Alute Mughwai amesema mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) anatarajiwa kupelekwa nje ya Kenya kufanyiwa matibabu ya viungo.
Wakili Mughwai ambaye ni kaka wa mbunge huyo alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana. Alisema mazoezi ya viungo ni muhimu kwake katika hatua hii ili kuepusha viungo kukakamaa.
Aliongeza kwamba akirejea nchini, Lissu atakwenda Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuwashukuru madaktari na wauguzi waliompatia huduma ya kwanza baada ya kushambuliwa kwake na kuwashukuru watu waliomtolea damu.
Baadaye atakwenda misikitini, makanisani kuwashukuru waumini kwa kumwombea na kumshukuru Mungu kwa kufanya muujiza huo kwake. Aidha alisema ataenda bungeni kuwashukuru wabunge na kuwashukuru wananchi wote waliomchangia damu na gharama za matibabu yake. Hata hivyo, alisema ataendelea kufaya kazi za siasa na sheria akiendeleza pale alipoachia kwa kasi zaidi.