- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LIPUMBA APATA PIGO LINGINE MAHAKAMANI
Dar es salaam: Mahakama kuu ya Tanzania imeipiga marufuku bodi ya udhamini ya CUF iliyokuwa imeundwa na Mwenyekiti wa CUF anayetambulikia na msajili wa vyama vingi vya siasa nchini Prof. Ibrahimu Lipumba kwa madai ya kuwa kwa sasa haiko kisheria
Naibu Mkurugenzi Uwenezi wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Maharagande amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa leo Disemba 19, 2017 mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera katika Mahakamu Kuu Dar es Salaam ambapo Jaji Dyansobera ameitaka bodi hiyo inayodaiwa kuwa ni bodi feki kutojishughulisha na kazi zozote za taasisi ya CUF.
Mahakama imepiga marufuku kwa bodi hiyo kufanya shughuli zozote zinazoihusu CUF mpaka pale shauri la msingi litakapomalizika.
Awali, mahakama iliyatupilia mbali maombi ya Advocate Mashaka Ngole(anayemuwakilisha Lipumba) ya kumuomba Jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa Lipumba anakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF.Mahakama Kuu imesema, hakuna hoja za kisheria zinazoizuia kuacha kuendelea na shughuli ilizozipanga.