- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LIPUMBA AKWAMA MAHAKAMANI TENA, ANYIMWA FEDHA ZA RUZUKU
Dar es salaam: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, imemzuia Jaji Francis Mutungi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini au Wakala wake yeyote yule kutoa fedha za ruzuku za chama cha wananchi CUF na kumpa Lipumba mpaka hapo mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani yatakapo sikilizwa na kutolewa maamuzi.
Maamuzi hayo yametolewa Leo tarehe 29 Mei 2018 na Jaji WILFRED DYANSOBERA katika mahakama hiyo na kusisitiza kuwa maombi ya CUF ya kulinda fedha hizo yana nguvu za kisheria.
Taarifa za chama zinaeleza kuwa Hadi Amri hii ya mahaka inatolewa, Jaji Mutungi na Ofisi yake (Msajili wa Vyama) imeshamruhusu Lipumba kuchukua zaidi ya Shilingi Bilioni 1.5 (Milioni 1,500) na fedha hizo zimekuwa zikiwekwa kwenye akaunti zisizotambuliwa na Bodi Halali ya Udhamini na kisha kuhamishiwa kwenye akaunti za watu binafsi akiwemo Lipumba Mwenyewe.
Shauri juu ya uhalali wa Bodi ya wadhamini linaendelea kusikilizwa na inatarajiwa kuwa shahidi wa tatu wa upande wa Chama ataanza kutoa ushahidi wake mwezi Juni mwaka huu.