Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 12:47 pm

NEWS: LIPUMBA AKUBALI KUACHIA UWENYEKITI CUF

Dar es Salaam: Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kwasasa yuko tayari kuachia madaraka ya chama hicho iwapo atapatikana mgombea mwenye sifa za uwenyekiti


Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 25, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Lipumba amesema muda ukifika wa uchaguzi hakuna sababu ya yeye kung'ang'ania madaraka.
"Nitampisha atakayekuja kuwania nafasi ya uenyekiti ilimradi tu awe na sifa za uenyekiti na akubalike kwenye chama,"amesema


Lakini amesema mpaka sasa hakuna mtu aliyejitokeza kuwania uenyekiti wa chama hicho ambaye atapitishwa pia kuwa mgombea urais 2020.

"Hata wewe mwandishi ikiwa unataka kuwania nafasi yangu karibu sana,ilimradi tu uwe mwanachama na sifa za kuwa mwenyekiti,"amesema Lipumba


Amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kutajwa kuitwa Chadema haitakidhuru chama hicho kwa sababu CUF bado inakubalika Zanzibar.
Amesema kwamba chimbuko la CUF ni Zanzibar, hivyo Chadema hawawezi kuiua CUF Zanzibar