Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:48 am

NEWS : LIBYA YAANZA UCHUNGUZI KUHUSU TAARIFA ZA BIASHARA YA WATUMWA MJI MKUU WA TRIPOL

Libya yaanzisha uchunguzi kuhusu biashara ya utumwaLibya yaanzisha uchunguzi kuhusu biashara ya utumwa

Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu suala la kushikiliwa na kuuzwa wahajiri kama watumwa karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Ahmed Maiteeq amesema kuwa, serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imeiagiza kamati iliyoundwa kuchunguza uuzaji wa wahajiri wa Kiafrika kama watumwa nchini humo ili kuwatia mbaroni na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa magendo ya binadamu.

Wahajiri wa Kiafrika ambao hatima yao ni kuuzwa kama watumwa huko Libya

Ripoti za hivi karibuni zimefichua kuwa raia wa nchi za Kiafrika ambao wamekuwa katika jitihada za kuelekea Ulaya wakikimbia mchafuko na hali duni ya maisha huuzwa kama watumwa wakiwa njiani huko Libya. Ripoti hizo zimesababisha radiamali kali kimataifa.

Wakazi wa Paris mji mkuu wa Ufaransa karibu elfu moja juzi usiku waliandamana kulalamikia magendo hayo ya binadamu na kuuzwa wahajiri kama watumwa huko Libya.