Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:48 am

NEWS: LEMA ATAKA KUFANYIKA MKUTANO WA VYAMA VYA UPINZANI

Arusha: Mbunge wa Arusha mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Godbless Lema ametoa Rai ya kufanyika haraka kwa mkutano wa wabunge wote wa vyama vya upinzani nchini Tanzania ili kujadili mustakabali wa Taifa hasa kutokana na kuendelea matukio ya ukiukwaji wa haki za binaadamu na hivyo hofu kutawala nchini.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 2, 2018 na waandishi wa habari jijini Arusha, Lema amesema mkutano huo, utasaidia kujadili kupigania uhuru wa kujieleza na kutoa maoni katika nchi kwani sasa ni vigumu kujitokeza hadharani kupigania haki kwani vitisho vilianza bungeni hadi sasa mitaani. "Kikao hiki kifanyike Dodoma ama Dar es Salaam, tuzungumze masuala ya kupigania haki na baada ya hapo tuje na msimamo wa pamoja na hii ni wabunge na viongozi wa vyama vyenye wabunge," amesema.

Amesema lazima ipatikane njia sahihi, kupigania haki kwani bila kukaa pamoja hali itaendelea kuwa mbaya na taifa litaharibika. "Mwanzo tulipokuwa tunakamatwa sisi wanasiasa watu waliona ni mambo ya kisiasa, alipopigwa risasi (Tundu) Lissu wengi waliona ni siasa, baadaye wameanza kukamatwa wanahabari hapo kupotezwa sasa wafanyabiashara vilio kila kona lazima sote tuungane na kusema hapana" amesema. Amesema uchumi wa taifa unaelekea kuyumba na miaka michache ijayo hali itakuwa mbaya sana kama hatua za haraka zisipochu