Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 8:32 pm

NEWS: LEMA APINGA VIKALI KAULI YA GAVANA KUTUMIA WANAJESHI

Arusha: Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amepinga vikali hoja za Gavana wa Benki Kuu,Profesa Florens Luoga zakwamba walitumia askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika operesheni ya maduka ya kubadili fedha, kwa kuwa kulikuwa na uhaba wa polisi, kwasababu Polisi wengi walikuwa kwenye kusimamia mitihani.

Mwanzoni mwa wiki hii BoT iliendesha operesheni ya kukagua maduka ya kubadilisha fedha mjini Arusha ikitumia maofisa wake na askari wa JWTZ mapema wiki hii, jambo ambalo limepingwa na wadau ambao wanasema jeshi liachwe lifanye kazi zake.

Lema, ambaye alikuwa mmoja wa watu walioandika mtandaoni kuonya dhidi ya matumizi hayo ya wanajeshi, amewaambia waandishi wa habari leo (Novemba 21) kuwa ni kosa kubwa kutumia jeshi katika mambo ya kiraia.

Amesema si kweli kuwa kulikuwana uhaba wa polisi.

"Arusha shule za serikali zilizokuwa na mitihani ni 24 na shule binafsi 49 hivyo kulikuwa na polisi wa kutosha," alisema Lema, ambaye ni waziri kivuli wa Wizara ya mambo ya Ndani bungeni.

Amesema hapingi operesheni ya BOT, lakini amesema njia iliyotumika haikuwa sahihi, imevunja sheria na imewawatisha wananchi, wawekezaji na wafanyabiashara.

"Jambo hili lina hatari kwa taifa. Hii opetesheni ingefanywa na polisi (au) hata mgambo na si kutumia vikosi vya jeshi. Kulikuwa na askari wa kutosha Arusha," amesema mbunge huyo.