Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:29 am

NEWS: KUTANA NA NESI ALIYEUWA WAGONJWA 100

Nesi mmoja kwa jina Neils Högel Wa kijerumani amekubali mbele ya mahakama kuwaua wagonjwa zaidi ya100, nchini Ujerumani katika hospitali mbili tofauti hali inayomfanya kuingia kwenye rekodi ya miongoni mwa wauaji wakubwa kabisa kuwahi kutokea.

Taarifa kutoka idara za upelelezi zinasema vifo hivyo vilitokana alikuwa akiwapatia wagonjwa wake dozi kali ambazo zilipelekea umauti wao katika hospitali mbili ambazo alikuwa akifanya kazi.

Lengo la nesi huyo, kwamujibu wa wapelelezi ilikuwa ni kuwashangaza na kuwavutia wafanyakazi wenziwe kwa kuwarejeshe fahamu wagonjwa aliowalaza kwa kotumia dozi kali. Mchanganyiko huo wa dozi za kuwalaza na kuwaamsha ndio uliowaathiri zaidi wagonjwa.

Lakini tayari nesi huyo yupo ndani kwa kifungu cha maisha jela kwa kesi ya kuuwa Raia 2 nchini humo kabla ya kesi hiyo.

Högel alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akimdunga mgonjwa sindano ambayo hakuandikiwa katika mji wa Delmenhorst.Mwaka 2008 alihukumiwa kwenda jela kwa miaka saba kwa kosa la kujaribu kufanya mauaji.

Kati ya mwaka 2014-15, alishitakiwa na kukutwa na hatia ya mauaji ya wagonjwa wawili na jaribio la kuua wagonjwa wengine wawili ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha.

Aliiambia mahakama kuwa anaomba radhi ya dhati na anatumaini kuwa ndugu wa marehemu hao wangepata utulivu na amani. Alijitetea kuwa maamuzi yake ya kuwadunga wagonjwa sindano za sumu hayakuwa ya kupanga.

Hata hivyo, katika kesi hiyo alikiri mbele ya daktari wa akili wakati wa kesi hiyo kuwa aliua zaidi ya wagonjwa 30.

Baada ya hapo wapelelezi wakatanua wigo wa uchunguzi wao kwa kufukua miili ya wagonjwa 130 ambao walipitia mikononi mwake.