Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:39 am

NEWS: KUTANA NA MTANZANIA MWANAMKE MKURUGENZI WA UN AKITOA SOMO LA KUJITAMBUA

Dar es salaam: Joyce Msuya ni Mtanzania Mwanamke ambaye ni Naibu Mkurungezi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP jana alitoa somo kwa viongozi wa vikundi mbalimbali vya wanawake akikazia mkazo swala la kujitambua na kutambua nini mahitaji yako ni moja ya chanzo cha mabadiliko yanayohitajika katika maisha.Naibu Mkurugenzi UNEP

Bi Joyce alisema hayo wakati akizungumza na wanawake mbalimbali waliofika kusikiliza historia yake na jinsi alivyoweza kumudu maisha ya mama, mke na mfanyakazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa na kupanda ngazi.

Aidha alisema pamoja na kujitambua mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kuwajibika, kujisukuma zaidi katika kazi na kufanya maamuzi ya kushirikisha familia hasa patna.

Msuya ambaye alianza kazi ya UNEP mwaka huu mwezi wa nane baada ya kupitia Benki ya dunia na mashirika mengine kadhaa alisema mfumo wa Tanzania wa shule, malezi ndiyo iliyofanya kuunganisha nguvu, uwezo na ujasiri wa kuweza kufanya mambo ambayo yamemfanya kupata nafasi kubwa zaidi.

Alisema mfumo wa Tanzania wa maisha umekuwa msukukumo mkubwa kwake kwani aliweza kuishi na watu tofauti na kuvumilia huku akitekeleza wajibu wake kwa kujiongeza zaidi.

Alisema kutokana na juhuzi za wazazi wake katika kusimamia malezi aliweza kupata maarifa zaidi ya kuishi kwa kuhudhuria shule za umma za Forodhani, Jangwani na Weruweru kisha kuchukua mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na kumalizia mafunzo hayo Mlalakua.

“Ukweli ni kuwa wazazi wangu walitaka tuishi maisha ya kawaida kama watanzania wengine ndiyo maana walinipeleka shule za bweni na kuhakikisha naenda jeshini. “ alisema Mkurugenzi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.