Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 12:48 pm

NEWS: KUBANA MAFUTA KWENYE MATENKI KULISABAISHA MV NYERERE KUKOSA BALANCE

Wazamiaji wanaoshughulika na uakoaji wa kivuko cha Mv Nyerere wamedai kuona dalili za hujuma zilizofanywa na baadhi ya watendaji wa kivuko cha MV Nyerere kilichozama Septemba 20 wakati kikitoka eneo cha Bugorola kisiwani Ukerewe kwenda Ukara,

Ambapo zaidi ya watu 227 walikufa katika kivuko hicho kilichozama kikiwa kimebakiza takribani mita 100 kufika mwisho wa safari yake kisiwani Ukara.

Wakizungumzia vitu walivyoviona wakati wakiendelea na hatua ya kunyanyua kivuko hicho jana, baadhi ya wazamiaji hao walisema wamebaini kuwa matanki ya uwiano (Balance tanks) yalikuwa hayajajazwa maji kama inavyotakiwa.

Walisema sababu za kutojazwa maji matanki hayo ni pamoja na kubana mafuta yanayotumika kwenye kivuko na kutumia matanki hayo kubebea mizigo kuliko uwezo wa kivuko.

Hivi sasa wataalamu wa uzamiaji, uokoaji na vyombo vya majini wanaendelea na kazi ya kukiibua kwenye maji kabla ya kuvutwa hadi nchi kavu.