- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA YAAPA KUTOHARIBU ZANA ZAKE ZA KINYUKLIA
Utawala wa Korea Kaskazini umesema hauko tayari kuharibu zana zake za kinyuklia iwapo kutaendelea kuwepo kwa vikwaza vya kibiashara dhidi yake.
Akiongea kwa niaba ya Serekali ya Korea kaskazini Ri Yong-ho aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa vikwazo hiyvo vinapunguza imani yake kwa Marekani.
Siku za hivi karibuni Korea Kaskazini imerejelea wito wake wa kuitaka Marekani na Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo na imeungwa mkono kutoka China na Urusi.
Lakini uongozi wa Trump unasema kuwa vikwazo hivi vitadumu hadi pale Korea Kaskazini itaharibu zana zake za nyuklia.
"Bila ya imani kwa Marekani hatuwezi kuwa na uhakika kwa usalama wetu wa kitaifa na katika hali kama hiyo hakuna vile tutaharibu silaha zetu kwanza."
"Imani kuwa vikwazo vinaweza kuchangia sisi kusalimu amri ni ndoto," aliongeza.