- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA YA KASKAZINI YASEMA YENYEWE NITISHIO KWA MAREKANI KWASASA
kiongozi wa Korea Kaskazini , Kim Jong-un, amesema taifa lake linawakilisha tishio kubwa la nyuklia kwa nchi ya Marekani. kauli hiyo ya kiongozi wa taifa hilo ikiwa ni siku ambayo baraza la usalama la Umoja wa mataifa linapiga kura kuidhinisha vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini,
Katika hotuba aliyoitoa kiogozi huyo kupitia shirika la utangazaji la habari nchini (KCNA) Kim amesema kuendelezwa kwa haraka kwa mpango wa nchi yake wa nyuklia kunashinikiza ushawishi muhimu katika siasa za kimataifa.
Azimio la hivi karibuni la baraza la usalama la Umoja wa mataifa linalenga kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zote za mafuta kwenda Pyongyang na kuitisha kurudishwa kwa raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika nchi za nje katika muda wa mwaka.
Korea Kaskazini imetaja nakala za usalama za Marekani zinazosisitiza kuhusu utumizi wa mabavu dhidi ya Pyongnyang kuwa za kihalifu, vyombo vya habari vya taifa hilo zimesema.
Wizara ya maswala ya kigeni ilimlaumu rais wa Marekani Donald Trump kwa kutaka kukandamiza ulimwengu kupitia sera yake mpya ya usalama.
Siku ya Jumatatu rais Trump alisema kuwa Washington lazima ikabiliane na changamoto inayoletwa na mpango wa kutengeza silaha wa Pyongyang.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini amesema kuwa mpango mpya wa Marekani kuhusu usalama hauna lolote bali mpango wa kutaka kutumia nguvu kulingana na chombo cha habari cha kitaifa KCNA.
Ameilaumu Marekani kwa kutaka kujaribu kuvuruga taifa hilo na kugeuza rasi yote ya Korea kuwa eneo litakalotawaliwa na Marekani.
Siku ya Jumatatu rais Trump alielezea kuhusu mpango huo mpya akiikosoa Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia licha ya shutuma kutoka Marekani na Umoja wa Mataifa.