Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:39 am

NEWS : KOREA KUSINI YAMUONYA TRUMP KWA MASHAMBULIZI KOREA KASKAZINI BILA RIDHAA

Korea Kusini yamuonya Trump juu ya kuishambulia Korea Kaskazini bila ya ridhaa yakeKorea Kusini yamuonya Trump juu ya kuishambulia Korea Kaskazini bila ya ridhaa yake

Mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini, amesema kuwa haiwezekani Rais Donald Trump wa Marekani kutumia chaguo la kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini bila ridhaa yake.

Bi Chu Mi-ae aliyasema hayo Jumatano ya jana akiwa mjini Washington na kuongeza kwamba, mara nyingi Trump amekuwa akisisitiza kuwa machaguo yote dhidi ya Korea Kaskazini yako mezani, lakini Marekani haitakiwi kutumia chaguo lolote la kijeshi dhidi ya Pyongyang, bila idhini ya nchi yake.

Bi, Chu Mi-ae, mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini

Mkuu huyo wa chama tawala nchini Korea Kusini sambamba na kusisitizia umuhimu wa kutumika njia za kisiasa kwa ajili ya kutatuliwa mgogoro wa eneo la Korea amesema kuwa, vitisho vya kijeshi dhidi ya nchi hiyo jirani (Korea Kaskazini) vitaendelea kuifanya hali ya mambo eneo hilo kuwa mbaya zaidi. Licha ya kukaribia miezi miwili bila serikali ya Pyongyang kufanya jaribio lolote la silaha za nyuklia au kombora, hadi sasa bado Marekani haijapunguza hatua zake za uhasama dhidi ya nchi hiyo, suala ambalo linaonekana kuwakera hata waitifaki wake wa eneo la Peninsula ya Korea.

Rais Donald Trump anayetajwa kuwa mpenda vita

Wiki iliyopita akiwa nchini Korea Kusini na katika safari yake ya kiduru barani Asia, Trump alitoa vitisho vya kutumiwa nguvu kubwa ya kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini. Kufuatia hali hiyo, siku chache zilizopita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini alinukuliwa akiikosoa Washington kwamba, hatua ya kupenda makuu Marekani katika suala la namna ya kukabiliana na Korea Kaskazini, imepelekea kutofikiwa maendeleo katika mazungumzo na Pyongyang.