- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YASEMA HAITAWEZA KUIBEMBELEZA MAREKANI
Kiongozi wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini Bw. Choe Son-hui amemshutumu vikali Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence na kumwita "mjinga" na ameonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo baina ya marekani na Korea yatafeli.
Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo.
hivi karibuni koera na Marekani zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.
Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia.
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.
Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita.
Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea Kaskazini, taifa la nyuklia na Libya, ambayo anasema ilikuwa na vifaa vichache tu ilivyokuwa ikicheza navyo.
"Kama mtu ambaye nimehusika kwenye masuala ya Marekani, siwezi kuficha mshangao wangu kufuatia matamshi kama hayo ya kijinga yanayotoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani," alisema.