- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KOREA KASKAZINI YARUSHA TENA KOMBORA KUBWA LA MASAFA MAREFU
Pyongyang: Korea Kaskazini imefanikiwa kurusha kombora la masafa marefu la ICBM lililoruka juu zaidi. Waziri wake wa Ulinzi wa marekani James Mattis amesema Korea Kaskazini inaendelea kurusha makombora yanaoonekana kuhatarisha usalama Duniani.
James Mattis amesema kuwa kombora hilo liliruka juu ikilinganishwa na kombora jingine lolote lile hapo awali.
''Korea Kaskazini ilikuwa ikiunda kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine ambalo linaweza kurushwa eneo lolote lile duniani'', Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema.
Kwa mujibu wa maafisa wa jeshi la Korea Kaskazini, kombora hilo liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960.
Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya hivi karibuni.
Hata hivyo jumuiya ya kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa na Marekani wameendelea kukosoa hatua hizo za Kora Kaskazini wakitaka hatua kali zaidi zichukuliwe.
Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake lililokuwa la sita la nguvu za kinyuklia ni mwezi Septemba.