Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:41 am

NEWS: KIPA WA LIVERPOOL ATISHIWA MAISHA HUKO UINGEREZA BAADA YA KUFUNGISHA MABAO 2

England: Kipa nambari Moja Kwasasa wa Majogoo wa jiji la Liverpool Loris Karius ameendelea kupokea vitisho kutoka kwa mashabiki mbali mbali wa soka Duniani hasa wale waishiayo nchini Uingereza hii ni baada ya kuwazawadia Miyamba ya soka nchini Uhispania Real Madrid Mabao 2 katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya yaliyopeleka msiba mzito kwa mashabiki Liverpool duniani kote hivyo kufanya Madrid kushinda taji lao la 3 mfululizo kwenye mashindano hayo.

Polisi wa eneo la Merseyside, nchini Uingereza ambapo anatokea kiba huyo wamesema wanafahamu kuhusu vitisho vya maisha ambavyo vimetolewa dhidi ya mlinda lango huyo na wanachukuwa tahadhari zote

'' vitisho vyovyote vinavyotolewa kupitia mitandao ya kijamii vinafaa kuchunguzwa.'' alisema afisa mmoja wa Polisi

Tunachukulia ujumbe huu wa vitisho kwenye mitandao ya kijamii kwa uzito sana. Visa hivi vitachunguzwa," polisi wamesema.

"Maafisa wa polisi wanafahamu kuhusu ujumbe kadha na vitisho vilivyotolewa kupitia mitandao ya kijamii.

"Polisi wa Merseyside wangependa kuwakumbusha wanaotumia mitandao ya kijamii kwamba makosa yooyte yakiwemo kutoa mawasiliano yenye hila na kutumia vitisho, haya yote yatachunguzwa."

Mjerumani huyo alimpa mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema bao rahisi la kwanza mjini Kiev.

Baadaye, alimruhusu Gareth Bale kufunga bao la tatu la Real kutoka mbali alipojaribu kuzuia kombora lake lakini likapita mikono yake na kutumbukia wavuni.

Hilo liliwawezesha Real kushinda taji la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya tatu mtawalia.

Baada ya kipenda cha mwisho kupulizwa, mlinda lango huyo alionekana kusikitika na kutokwa na machozi.

Baadaye, aliwaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo ya Anfield.

Mlinda lango mwenzake Liverpool Simon Mignolet amemtetea Karius na kusema atajikwamua kutoka kwa masaibu hayo ya fainali hiyo ya Uefa.

"Iwapo anataka kuzungumza, bila shaka nitakuwepo," alisema Mbelgiji huyo aliyekuwa kwenye benchi wakati wa mechi hiyo.

"Kila kipa anamuelewa.

"Nimewahi kujipata katika hali kama hii mwenyewe awali na hayo ni mambo ambayo huwa unakumbana nayo.

"Kitu pekee nilichomwambia ni kwamba kuna sababu iliyotufanya kufika fainali, na kuna sababu yetu kucheza kwenye fainali, hivyo fikiria hilo.

"Lakini bila shaka, ni jambo ngumu sana kumwambia chochote na kumwacha atulie na kuelewa.