Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 6:32 am

NEWS: KIONGOZI MKUU WA UPINZANI MOISE KATUMBI AKATALIWA KUKANYAGA CONGO

Kiongozi wa upinzani Moise Katumbi alikataliwa kuingia DRC kupitia mpaka na Zambia Ijumaa wakati alipojaribu kurejea kutoka uhamishoni ili kuwasilisha fomu yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Kiongozi huyo wa upinzani alizuiwa kurejea nyumbani ameahidi kupambana ili kufanyika uchaguzi halisi.

Moise Katumbi , mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga , alizuiliwa kuingia katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kushitakiwa kwa makosa dhidi ya usalama wa taifa, maafisa wamesema. Katumbi mwenye umri wa miaka 53, amekuwa akiishi uhamishoni alikomua binafsi nchini Ubelgiji tangu Mei 2016 baada ya kutofautiana na rais Joseph Kabila, ambaye ameitawala DRC kwa miaka 17.

Alipanga kurejea nchini humo kwa ndege ya binafsi kutoka Johannesburg kwenda Lubumbashi, mji mkuu wa jimbo la Katanga, kuwasilisha fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu mwezi Desemba, hatua ambayo itaongeza mbinyo kwa rais Kabila.

Lakini meya wa mji wa Lubumbushi alimkatalia ruhusa ya kuingia, wakati ofisi ya mwendesha mashitaka imesema Katumbi ameshitakiwa kwa "kuhatarisha usalama wa ndani ya nje" na atakamatwa iwapo atarejea. Mwandishi habari wa redio ya Ufaransa RFI amesema Katumbi badala yake aliwasili katika mpaka wa Zambia na DRC wa Kasumbalesa

Vidio zilizowekwa katika mtandao na wasaidizi wake pamoja na watu wengine zinamuonesha akiwa katika upande wa mpaka wa Zambia, akisalimiana na mamia ya waungaji wake mkono katika gari yake.

"Serikali inanizuwia kutua na inafunga mpaka, uhalifu wangu? Kutaka kuingia nchini mwangu na kuwasilisha fomu za kuomba urais," Katumbi aliandika katika ukurasa wa Twitter.

"Kwa kujaribu kunizuwia, wanataka kuwanyima Wakongo haki yao ya uchaguzi halisi. Nitapambana," ameongeza.