Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:47 pm

NEWS: KINACHOENDELEA KWA SASA KWENYE UCHAGUZI NCHINI KENYA

Nairobi: Leo wakenya wanapiga kura licha ya kuwepo kwa hali ya mvutana kati ya Muungano wa upinzani NASA na chama tawala chake Uhuru kenyatta.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa katika uchaguzi mpya wa urais unaofanyika huku wapiga kura wakiwa wamegawanyika baada ya kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga kuwataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo.

Jijini Nairobi, katika mitaa ya Mathare Dereva taxi David Njeru amesema katika uchaguzi wa mwanzo kulikuwa na misururu mirefu ya wapiga kura, tofauti na ilivyo sasa hivi.

Katika mji wa Kisumu ambayo ni ngome ya Odinga, hakuna kinachoendelea. Hakuna aliyejitokeza kama ilivyokuwa mwezi Agosti.

Hata hivyo, katika ngome za Jubilee kama Nyeri, Kiambu na maeneo kadhaa ya jiji la Nairobi, wapiga kura wamejitokeza kupiga kura.

Maafisa wa usalama wanaonekana wakipiga doria maeneo mengi nchini humo.

Wachambuzi wa siasa wanasema, Uchaguzi huu umewagawa Wakenya na kuna umuhimu wa kushughulikia mgawanyiko huu baada ya Uchaguzi huu tata.

wananchi wa kenya wakisubiri kuingia ndani kupiga kura

Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta, amepiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei eneo la Turbo mjini Eldoret magharibi mwa Kenya.

wananchi kenya wakiendelea na zoezi la kupiga kura licha kunyesha kwa mvua.