Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:45 am

NEWS: KIM JONG-UN ASISITIZA KUWA YUKOTAYARI KUKUTANA NA TRUMP

Rais wa korea kaskazini Kim Jong Un, amekutana leo na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, nakutoa ujumbe kuwa uongozi wa Korea Kaskazini bado unania na mkutano wake na rais wa Marekani Donald Trump kuendelea mwezi ujao nchini Singapore kama ilivyopangwa, Aidha amesema bado anania ya kutokuwa na maeneo ya kutengeza silaha za nyuklia.

Kauli hii ya kiongozi huyo wa Kaskazini, imekuja wakati huu rais Trump akisema bado wanaendelea kuzungumza na maafisa wa Pyongyang na huenda mazungumzo hayo yakaendelea kama ilivyopagwa.

Wiki hii, rais Trump alijiondoa kwenye mazungumzo hayo, baada ya kusema kuwa, matamshi yenye ukali na yaliyoonekana kuwa ya chuki, kutoka Korea Kaskazini yasingemwezesha kuja katika meza ya mazungumzo.

Hata hivyo, matamshi ya rais Trump siku ya Jumamosi kwamba mambo yanakwenda vizuri, huenda viongozi hao wakakutana tarehe 12 mwezi Juni kama ambavyo ilikuwa imepangwa.

Korea Kaskazini pamona na kutaka mkutano huo, imeonekana kutokubaliana na msimamo wa Marekani kuwa iachane kabisa na mradi wake wa nyuklia, suala ambalo linaendelea kuwa tata.