- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIM AIONYA MAREKANI KWENYE HOTUBA YA MWAKA MPYA
kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameionya Marekani dhidi ya kusisitiza hatua za upande mmoja, vinginevyo, watatafuta njia nyingine ya kuendelea na mipango yake ya Kibabe.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya kwa taifa lake, Kim Jong Un amesema anataka kuendeleza mazungumzo na Marekani kuhusu kuondoa silaha za nyuklia kwenye Ras ya Korea, lakini akatoa tahadhari, akisema hawataki uwezo wao wa kuwa na subira uwekwe majaribuni.
Kiongozi huyo wa kiimla amesema katika hotuba yake, kwamba anataka mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini yasifanyike tena, na Marekani iache kuweka silaha za kivita nchini Korea Kusini.
Ameonya juu ya uwezekano wa nchi yake kutafuta njia nyingine, ikiwa Marekani 'itaendelea kuvunja ahadi ilizozitoa, na kubeza subira ya watu wa Korea Kaskazini, kwa kuwataka wachukue hatua kadhaa wakati ikiendeleza vikwazo na shinikizo' dhidi ya nchi yao.
''Ikiwa Marekani haitatimiza ahadi ilizozitoa mbele ya macho ya ulimwengu mzima,'' amesema Kim, ''tunaweza kukosa chaguo jingine mbali na kufuata njia mpya katika kulinda uhuru wetu na kutetea maslahi yetu.''