Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 12:44 pm

NEWS: KILA BAADA YA DAKIKA 5 MWANDISHI MMOJA HUPOTEZA MAISHA.

DOM: Takwimu zinaeleza kuwa kila baada ya dakika tano mwandishi wa habari mmoja duniani hupoteza maisha kutokana na usalama wao kuwa hatarini.

Hayo yamebanishwa leo jijijini Dodoma na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka Shirika la Elimu,la Umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu Sayansi na Technologia, (UNESCO) Chritina Musagoroche wakati akiwasilisha taarifa iliyotolewa na Shirika kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Amesema kuomeongezeka visa na vitisho na mashambulizi dhidi ya waandishi na kudai kuwa takribani waandishi 800 na 25 wameuwawa Duniani kote ukiondoa wale wanaofia vitani .

Aidha amefafanua kuwa mwaka 2016 waandishi 76 wamepoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao.

Katika Mafunzo ya shirika hilo yalikuwa na lengo la kuangazia haki na usalama wa wanahabari,kazini,,pamoja na kuwahamasisha wanahabari kuhusu haki zao, na haja ya kuwa na uelewa kuhusu usalama wao kazini.

Ikumbukwe kuwa sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, baada ya kukamilika kwa kanuni zake za mwaka 2017, inamtambua kuwa sifa za mwandishi wa habari ni pamoja na kuwa na Diploma ya Taaluma hiyo.