- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIGWANGALLA ATOA SIKU 30 WAMILIKI WA MAGOGO BANDARINI
Dar es salaam: Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) Jana (03.12.2017) ametoa muda wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s Salaam ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza ili mara moja kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini hapo kwa muda wa miaka 10 sasa.
Dk.Kigwangalla ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini hapo kukagua mali na bidhaa zinazoshughulikiwa na Wizara yake hiyo ambapo katika zkukagua kwake huko alibaini uwepo wa makontena hayo 55 ambayo yapo kwa miaka 10 sasa yakihifadhiwa huku wahusika wakishindwa kujitokeza.
“Naagiza mamlaka zilizo chini ya wizara yangu kuhakikisha wanahakiki magogo yote yalipo hapa bandarini. Mwenye huu mzigo lazima ajulikane hasa haya magogo 938, Ndani ya siku 30 mwenye haya magogo atangaziwe na ajitokeze vinginevyo itabaki kuwa mali ya Serikali” alisema Dk. Kigwangalla.
Hata hivyo aliagiza pia kontena 55 zilizokutwa bandarini hapo zenye magogo pia nazo wahusika wajitokeze na nyaraka zao kamili ili waeleze kama kweli wameyatoa Zambia magogo hayo ama sehemu gani hivyo wajitokeze na wasipofanya hivyo ndani ya siku hizo 30, magogo hayo yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Katika ziara hiyo, Waziri Dk.Kigwangalla aliweza kutembelea bandari ya Dar es Salaam pamoja na maeneo yanayohifadhiwa magogo hayo zikiwemo bandatri ya nchi kavu ya NASACO, Malawi (Malawi Cargo) na baadae eneo hilo la bandari ya Dar es Salaam.
Akiwa katika eneo la Malawi Cargo, Waziri Dk. Kigwangalla aliweza kushuhudia makontena mbalimbali yakiwemo yale ya mbao aina ya mitiki ambayo inatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi huku akibaini uwepo mkubwa wa udanganyifu kwa wasimamizi wa upakuaji na usafirishaji katika eneo hilo la bandari ambao awali walitaja idadi ndogo ya makontena ya mbao mbele ya Waziri hali iliyopelekea kuanza kuyakagua makontena yote ndani ya eneo hilo.