- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KHASHOGGI AWA MTU MWENYE USHAWISHI DUNIANI MWAKA 2018
Khashoggi alikuwa mwandishi maarufu na kinara wa kuikosoa serikali ya kifalme ya Saudia na aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2.
Watu wengi katika jamii ya kimataifa wanaamini Mauaji hayo yaliamuriwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman.
Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.
Khashoggi alikimbilia nchini Marekani akihofia maisha yake mwaka jana. Akiwa Marekani alikuwa akiandika makala kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo aliendeleza harakati zake za kumkosoa Mohammed bin Salman. Alienda Istanbul kushughulikia mchakato wa ndoa na mchumba wake wa Kituruki.
Rais wa Marekani Donald Trump amejaribu kuukingia kifua utawala wa Saudia na bin Salman. Shirika la ujasusi la CIA linadaiwa kuhitimisha kuwa bin Salman alihusika kwenye mauaji, japo Trump alidai kuwa CIA hawakutoa hitimisho hilo. Lakini maseneta wa Marekani wanaamini kuwa mwanamfalme huyo alihusika.