- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA YAPIGWA KALENDA TENA
Dar es Salaam: Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili viongozi tisa wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe umedai unasubiri uamuzi ya Mahakamani ya Rufaa.
Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, amedai hayo leo Alhamisi Januari 3, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
"Shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwa kuwa kuna amri ya kusitisha mwenendo wa kesi hii katika Mahakama ya Hakimu, hivyo tunasubiri uamuzi ya Mahakama ya Rufaa. Hivyo kutokana na hali hiyo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai Kadushi.
Wakili Kadushi baada ya kueleza hao, wakili wa utetezi, Profesa Abdallah Safari ameomba kujua endapo upande wa mashtaka kama wamewasilisha hati ya dharura katika Mahakama ya Rufaa.
Akijibu hoja hiyo, Kadushi amedai upande wa utetezi hawana uhalali wowote wa kuhoji suala hilo.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mashauri aliutaka upande wa utetezi kwenda kuhoji suala hilo Mahakama ya Rufaa.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 17, 2019, itakapotajwa.
Kati ya wa shtakiwa hao tisa, wawili ambao ni Mbowe na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Esther Matiko wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.
Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana zao Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kukiuka masharti ya dhamana.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 112/ 2018 ni wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Mnyika (Kibamba), John Heche (Tarime Vijijini), Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini).
Pia wamo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018 maeneo ya Dar es Salaam.