Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 2:44 pm

NEWS: KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA KUNGURUMA TENA LEO

Dar es salaam: Kesi na. 112/2018 inayowakabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko kuendelea kusikilizwa leo Desemba 21, 2018 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Mbowe na wenzao saba ambao ni viongozi wa chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini, wanakabiliwa na kesi ya jinai, Mahakama ya Kisutu, kwa mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi wa uasi.

Mbowe na Matiko walirudishwa rumande Baada ya Mahakama hiyo Ijumaa Novemba 23, 2018, kuwafutia dhamana kutokana na kukiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nje bila kibali cha Mahakama hivyo kushindwa kufika mahakamani siku ambazo kesi yao ilipangwa kwa usikilizwaji wa awali.

Uamuzi huo wa kuwafutia dhamana ulitolewa majuma mawili yaliyopita kufuatia maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka, Novemba 12, 2018.

washtakiwa hao kupitia kwa wakili wao, Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu, kupinga uamuzi huo, huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kupinga uamuzi huo, chini ya hati ya dharura.

Katika rufaa hiyo pamoja na sababu nyingine, walidai Mahakama ya Kisutu ilikosea kuwafutia dhamana bila kuwapa wadhamini wao taarifa ya kujieleza kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza.

Sababu nyingine walidai Mahakama ya Kisutu imekosea kuwafutia dhamana wakati walifika mahakamani wenyewe Novemba 12 bila kukamatwa na Ijumaa Novemba 23, 2018.

Vilevile walidai masharti ya dhamana aliyopewa ni kinyume cha sheria kwa kuwa hata mantiki au hata viwango vya kisheria.