Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:53 pm

NEWS: KESI YA RUSHWA YA RAIS ZUMA KUSIKILIZWA MEI 20

Hatimaye Mahakama ya Afrika Kusini imechukua uamuzi wa kuahirisha kesi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma hadi Mei 20, 2019.

Jacob Zuma anakabiliwa na mashitaka ya rushwa katika kesi kubwa ya mauzo ya silaha, karibu miaka ishirini iliyopita.

Jacob Zuma, aliripoti leo Ijumaa asubuhi akiwa peke yake bila kusindikizwa na polisi katika mahakama ya Pietermaritzburg.

Nje ya mahakama, mamia ya wafuasi wake walikja kumuunga mkono.

Baada ya nusu saa kesi hiyo ikianza, jaji Mjabulinesi Madondo aliamua, kwa ombi la wakili Jacob Zuma, kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 20 Mei 2019.
"Kesi inaahirishwa hadi tarehe 20 Mei 2019. Mtuhumiwa namba moja (Jacob Zuma) ataripoti mahakama saa 9:30 siku hiyo," amesema Jaji.

Mjabulinesi Madondo amesema watasikiliza mawakili wa washtumiwa wawili, Jacob Zuma na kampuni ya Ufaransa ya Thales, ambao wataomba kusitishwa kwa kesi hiyo.

Ikiwa Jaji atakubaliana na hoja hiyo, hakutakuwa na kesi.

Katika kesi hiyo, Zuma anashutumiwa kupokea rand 4,072,499.85 sawa na euro 260,000 (kwa bei ya sasa) - kama rushwa aliyopewa na kampuni ya Thales wakati wa mkataba wa mauzo ya silaha wa euro bilioni 4 mnamo mwaka 1999.

Wakati huo, Jacob Zuma alikuwa "waziri" wa serikali ya mkoa na kisha makamu wa rais wa Afrika Kusin.Jacob Zuma, mwenye umri wa miaka 76, ameendelea kukanusha mashtaka dhidi yake.