- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA RUFAA YA MBOWE NA MATIKO KUSIKILIZWA KESHO
Dar es salam: Mahakama Kuu ya Tanzania, imepanga kusikiliza shauri la madai ya kufutiwa dhamana lililofunguliwa mahakamani hapo na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, kesho Alhamisi asubuhi.
Jaji Rumanyika ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa kwa haraka.“Nataka shauri hili lisikilizwe haraka kama ambavyo waombaji walivyoleta maombi yao,” ameeleza Jaji Rumanyika.
Amesema, “mahakama hii, ni sharti izingatie ukweli kuwa kesi hii, imefunguliwa kwa hati ya dharura sana.
Hivyo basi, hatuwezi kuacha kusikiliza kesi hii kwa sababu itakuwa inakwenda kinyume na maombi yaliyoletwa.”
Kauli ya Jaji Rumanyika ilikuja kufuatia maombi ya upande wa mashitaka kutaka kesi hiyo isikilizwe Jumatatu ijayo.
Akiwasilisha maombi hayo mahakamani, wakili mkuu wa serikali, Faraja Nchimbi, alidai kuwa upande wa mashitaka hauko tayari kuendelea kesi hiyo, hadi itakapopewa mwenendo mzima wa kesi.
Akijibu madai hayo, Jaji Rumanyikwa aliagiza kesi hiyo kusikilizwa kwa kutumia mwenendo wa kesi ambao haujachapwa ili kulinda haki za waomba rufaa.
Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana tarehe 23 Novemba mwaka huu, kufuatia madai ya kuidharau mahakama na kukiuka masharti ya dhamana.