Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:42 pm

NEWS: KESI YA NAIBU JAJI MKUU KENYA YASIMAMISHWA KUSIKILIZWA

NAIROBI: Mahakama Kuu Kenya yasimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Jaji huyo alikuwa amewasilisha ombi mbele ya Jaji Chacha Mwita akimuomba asijibu mashtaka dhidi yake ya ulaghai, utumiaji mbaya wa mmalaka na kukwepa kulipa kodi.

Kupitia wakili Okongo Omogeni, alikuwa ameambia Mahakama Kuu kwamba kesi iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.Image result for Philomena Mwilu.

Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.

Alikamatwa Jumanne katika majengo ya Mahakama ya Juu na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu ambapo baadaye aliachiliwa huru kwa dhamana.