- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA KUCHAPISHA VIDEO ZA NGONO YA WEMA IMEHAIRISHWA
Dar es salaam: Taarifa kutoka katika mahakama ya Kisutu zinaripoti kuwa Upelelezi wa kesi ya kuchapisha picha na video za ngono na kuzisambaza kwenye mtandao ya kijamii inayomkabili msanii wa Bongo Move Wema Sepetu haujajamilika.
Hayo yamebainika leo Jumatano Novemba 21 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde.
Wakili wa Serikali, Jenipher Masue akiiwakilisha Jamhuri amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Baada ya Wakili Masue kudai hayo, mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Wema anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha picha za ngono na kuzisambaza katika akaunti yake ya Instagram.
Amedai kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika akaunti yake Instagram.