- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI YA BILIONEAN WA NYUMBA ZA LUGUMI "DR SHIKA" YAFUTWA
Dar es salaam: Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hawataendelea na kesi dhidi ya Dk Louis Shika kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo na hazijanunuliwa
Akizungumza na waandishi wa habari Jana jumatano (06.11.2017) Mambosasa amesema kesi yake haina mashiko hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara.
Amesema Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na kusababisha kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo. ββDk Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu tulisema tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko ndiyo maana hatuendelei nayo,β amesema Mambosasa.
Novemba 9 mwaka huu Kampuni ya Udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na moja Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni.