- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KESI PICHA ZA NGONO YA WEMASEPETU BADO KIZUNGUMKUTI
Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi inayomkabili Mrembo wa Bongo Move Wema Sepetu ya kujirekodi video na picha za ngono nakisha kuzisambaza katika mitandao ya kijamii bado haujakamilika
Hiyo imeelezwa leo Desemba 12, 2018 na Wakili wa Serikali, Mosia Kaima wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Wakili Kaima ameieleza Mahakama kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi wake bado haujakamilika.
Ameiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi wa shauri hilo utakuwa umekamilika ama la.
Baada ya wakili huyo kueleza hayo, wakili wa Wema, Ruben Simwanza alisema hana pingamizi.
Hakimu Masonde aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 28 mwakani na Wema yupo nje kwa dhamana.
Mwigizaji huyo wa filamu alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba Mosi mwaka huu kujibu shtaka hilo.
Hata hivyo baada ya kusomewa shtaka hilo na kukana alitakiwa kutoweka tena video zinazohusiana na ngono wala maneno yoyote yenye mwelekeo huo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Mshtakiwa huyo alipewa masharti hayo na Hakimu Kasonde wakati akipatiwa dhamana na kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh10 milioni. Wema alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.
Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa Oktoba 15 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wake wa Instagram.