- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : KENYATTA AWAOMBA WAKENYA KUJITOKEZA KWA WINGI
Naombeni wananchi mjitokeze kwa wingi-Kenyatta
Rais Kenyatta, kwenye hotuba yake kwa taifa jana kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo, aliwataka kujitokeza kushiriki uchaguzi wa leo.Alisema kila Mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote,pia aliwaonya wale walio na mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali haitawaruhusu.
Rais Kenyatta, kwenye hotuba yake kwa taifa jana kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo, aliwataka kujitokeza kushiriki uchaguzi wa leo.Alisema kila Mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote.Hata hivyo aliwaonya wale walio na mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali haitawaruhusu.
Ulinzi waimarishwa kwenye vituo vya kupigia kura
Ulinzi mkali umedumishwa kote nchini Kenya huku vituo vya kupigia kura vikitarajiwa kufunguliwa mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri.Uchaguzi wa leo wa marudio umesusiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.Maelfu ya maafisa wa polisi na walinda usalama wengine wametumwa, kulinda vituo vya kupigia kura.
Rais Uhuru Kenya, amewaomba raia wa nchi hiyo kutii haki yao ya kikatiba, na kujitokeza kupiga kura.Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati jana alisema serikali imemhakikishia kwamba kutakuwa na usalama wa kutosha vituoni.Aidha, alisema amehakikishiwa kwamba polisi hawatatumia ukatili.