Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:38 pm

NEWS: KENYATTA AAPA KUTOKUFANYA MAZUNGUMZO NA MPINZANI WAKE

Nairobi: Rais mteule wa kenya Uhuru Kenyatta amekataa kufanya mazungumzo yoyote na kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Raila Odinga ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Kenya.

Katika hotuba yake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio jana, Kenyatta amesema kuwa anaamini mpinzani wake mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kwa mara nyengine tena kupinga uchaguzi wake naye akajibu kuwa yupo tayari kufata sheria.

Kenyatta amewataka wapinzani wake wa Nasa kutumia njia zote za kisheria katika kupigania haki yao.

Wawacheni mwanzo watumie njia zote za kisheria zilizosalia wawacheni wafanye wanachotaka.

Hakuna mtu yeyote atakayewadhulumu haki yao ya kikatiba.

''Kuhusu ajenda yangu ya kusonga mbele nitazungumza baada ya makabiliano ya mahakamani yamekwisha'' , alisema Kenyatta katika makao makuu ya tume ya uchaguzi katika eneo la Bomas jijini Nairobi.

Rais Kenyatta pia alimshutumu Raila Odinga kwa kujiondoa katika uchaguzi huo.

''Licha ya kwamba mpinzani wangu mkuu alienda mahakamani akitaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali na akakubaliwa, aliamua kutotilia maanani uamuzi wote kwa pamoja ambao uliagiza kufanyika kwa uchaguzi katika kipindi cha siku 60 uliosimamiwa na IEBC.Baadaye alikaataa kushiriki katika uchaguzi''.

Katika uchaguzi wa marudio Uhuru alijipatia kura 7,483,895 huku Raila Odinga akijipatia kura 73,228 hata baada ya kujiondoa katika uchaguzi huo.