- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KENYA WANAPIGIA KURA MUSWADA WA KUONGEZA WANAWAKE BUNGENI
Wabunge nchini Kenya, wanapigia kura mswada muhimu, unaoleza kuwa thuluthi mbili ya jinsia moja, haistahili kutawala katika bunge la taifa na lile la Senate nchini humo.
Katiba ya mwaka 2010, iliweka wazi kuwa, nafasi za uteuzi katika mabunge hayo mawili, hazistahili kutawaliwa na jinsia moja, inayozidi thuluthi mbili.
Hata hivyo, Katiba hiyo haikueleza wazi namna ya kuepuka hali hiii, lakini Mwanasheria mkuu alikwenda katika Mahakama ya Juu, iliyoagiza bunge kurekebisha kifungu cha Katiba ili kutekeleza agizo hilo.
Mswada huu unaopigiwa kura, unabadilisha kifungu nambari 97 na 98 ili kuongeza idadi ya wanawake katika bunge hilo ambalo limetawaliwa na jinsia ya kiume katika historia ya siasa nchini humo.
Viongozi wa juu wa serikali, wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, wametoa wito kwa wabunge kuupitisha mswada huo ili kutoa nafasi kwa wanawake zaidi kuingia bungeni.
Kati ya wabunge 290 nchini Kenya, kwa sasa wabunge wanawake waliochaguliwa ni 22 na 50 wateule na kufanya idadi yao kufika 75. Iwapo mswada huu utapitisha idadi hiyo ya wanawake, inatarajiwa kuongezeka na kufikia zaidi ya 100.
Kenya ni ya mwisho katika ukanda wa Afrika Mashariki, kwa wanawake walio bungeni.
Rwanda ni ya kwanza kwa asilimia 61, Tanzania ni ya pili kwa asilimia 36 sawa na Burundi, huku Uganda ikiwa na asilimia 34 na Kenya ikiwa na asilimia 22.