Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:42 pm

NEWS: KAULI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUHUSU AJALI YA WATALII WANNE MKOANI ARUSHA

DOM: Wizara ya Maliasili na Utalii yasikitishwa na tukio la ajali ya watu sita Mkoani Arusha wakiwemo watalii wanne kutoka nchini Hispania na Italia.

Siku chache mara baada ya watu sita wakiwemo watalii wanne raia wa nchini hispania na italia kufariki dunia katika ajali baada ya gari la watalii hao kugongana na roli eneo Wilayani Monduli Mkoani Arusha,wizara ya maliasili na utalii nchini imeonyesha kusikitishwa na tukio hilo na kuwatoa hofu watalii wanaoingia nchini ambapo imeanza mikakati ya kushirikiana na mamlaka husika kuboresha miundombinu ya barabara zinazoelekea maeneo ya hifadhi za utalii nchini

Akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii wakati wakikabithiwa vifaa maalumu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano vyenye dhamani ya milioni mia moja Mkurugenzi wa idara ya Sera na Mipango kutoka wizara hiyo Dr Idd Mpunda amesema Wizara hiyo itaendelea kuwakikishia watalii wanaokuja nchini juu ya hali ya usalama na kwa sasa wanaimarisha miundombinu katika maeneo ya hifadhi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Kimarekani la Usaid Karolgn Upham amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na tanzania katika kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kulinda rasilimali hiyo ambayo ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani….bi karolgn upham mwakilishi usaid

Naye Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii Doreen Makaya ili kuendelea kukuza soko la utalii nchini wizara hiyo imejipanga katika kuimarisha mifumo mbalimbali ikiwemo ya kiteknolojia ili kuendelea kupokea idadi kubwa ya watalii kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.