Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:45 pm

NEWS: KAULI YA RAIS MAGUFULI YAWAPA KIBURI WAFUGAJI.

ITASWI KONDOA: Wafugaji wa kijiji cha Itaswi Kaata ya Itaswi Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma wameutuhumu uongozi wa kijiji akiwemo Diwani kwa madai ya kuwanyang'anya maeneo yao ya Malisho na kuyatumia kwaajili ya kilimo.

Shutuma hizo zimetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli kutoa maagizo kwa viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini kwa kushirikiana na wizara ya mifungo na uvuvi kuandaa mipango bora itakayowawezesha wafugaji kufuga mifugo yao bila kuwathiri wakulima.

Wakizungumza kwenye ziara ya Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kanda ya kati (singida na Dodoma) Dominic Bruno alipowatembelea kijijini hapo Moja wa wafugaji Ally Charles amesema Serikali iliandaa mipango na matumizi bora ya ardhi ambayo ilikuwa ikitumika siku za nyuma lakini cha kushangaza baadaye uongozi uliitisha mkutano na kudai kuwa mpango huo umesitishwa.

"Serikali iliandaa mipango miji ikatenga eneo la Chang'ombe, ilesi, ilesi msitu kwa ajili ya malisho ikaweka na bikoni lakini wakazuka viongozi wakenda kuvamia maeneo hayo na kuanza kuyalima tumeshafuatili mpaka kwa mkuu wa Mkoa lakini tunapigwa kalenda sasa hatuelewi uongozi huu unampango gani"amesema Charles.

Pia Jafari Hamisi amesema malisho yalikuwepo tokea enzi za babu zao isipokuwa kuna baadhi ya watu wachache wenye nia ovu wamevamia na ndio chanzo cha migogoro hiyo.

"Viongozi tuongee kwa kumwongopa mungu mitasali ipo na malisho yapo tusiongee kwa kumtetea mtu viongozi wetu ndo chanzo hamko makini tunashukuru rais kwa kusimama na kututetea sisi wafugaji wanyoge".

Akizungumzia tuhuma hizo diwani wakijiji cha Itaswi Said Chobu amekana tuhuma hizo na kudai kuwa si za kweli ningekuwa siwatumikia wananchi wasingenichangua kuwaongoza kwa kipindi chote cha miaka mine nikiwa Mwenyekiti hadi leo hii nimekuwa Diwani.

‘’Na mimi unaeniona hapa nimekuwa mwenyekiti vipindi vinne na bahati nzuri na haya yanayozungumzwa kwenye matumizi bora ya ardhi mimi ndiye niliyekuwa mwenyekiti mwaka 2002 mwaka huo kuna maaeneo yalikuwa yameanishwa na matumizi hayo sisi hatukuyaomba kama kijiji bali ni Wilaya yenywe iliamuwa na kuja kupanga maeneo wakafanya utafiti wakaweka na bikoni mwisho wasiku wakasema wameishiwa na fedha watarudi hadi sasa ninapoongea hawajarudi’’ ameongea Diwani huyo.

Akiongelea sakata hilo mwenyekiti wa kijiji hicho Issa Yusuph amesema si kweli na kudai kuwa anamiliki na kulima maeneo ambayo ni mali yake halimi shamba la mtu yoyote.

"Ni kweli serikali ilipanga mpango na matumizi bora ya ardhi kijijini tangu mwaka 2002 na waliweka bikoni lakini cha ajabu na cha kushangaza mpango huo haujakamilika hadi leo" amesema Mwenyekiti huyo.

Awali akizungumza Katibu wa CCWT Kanda ya kati (Singida na Dodoma )Dominic Bruno amewataka Wafugaji hao kufuga mifugo kwa wingi lakini kwa kufuata kanuni na taratibu za ufugaji ili kuwepo na mifugo mingi lengo ni kuongeza maligafi ambayo itasaidia kuendana na juhudi za serikali kuelekea Tanzania ya Viwanda.

’’Wafugaji au wakulima wanahitajiana ,wakulima wanawahitaji ng’ombe na wafugaji wanahitaji mazao ya kilimo, kwahiyo changamoto ni kwenu viongozi wa mikoa na wilaya kutengeneza mipango mizuri itakayowapa haki makundi yote kuishi bila migogoro’’amenukuu maneno ya Rais Katibu huyo.

Mbali na hayo amewataka kutumia mifugo hiyo kuwasomeshea watoto wao baadaye waweze kuwasaidia katika kuleta maendelea na kuweza kujikwamuwa kiuchumi.

Chama cha wafugaji Tanzania kilianza mwaka 2013 ikiwa na lengo la kutetea wafugaji hususani kwenye suala nzima la malisho, maji na miundombinu, kutoa elimu ya ufugaji bora na kuwaunganisha wafugaji kuwa na chombo cha kusimamia utetezi katika masilahi yao.

Ziara ya katibu huyo katika wilaya ya Kondoa ilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji bora na kufanya uchanguzi wa viongozi wa kata utakaokiwa unasaidia kuwawakirisha wafugaji katika kufikisha matatizo yao kwenye chama hata ngazi za juu.