Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:25 pm

NEWS: KATIBU ACT WAZALENDO AMFUNGULIA KESI RAIS MAGUFULI

Katibu mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Ado shaibu amemfungulia mashtaka Rais John Magufuli na mwanasheria mkuu wa Serekali Bw. Dk. Adelardus Lugango Kilangi kwa kile alichodai kuwa ameshindwa kutimiza masharti ya kikatiba tangu kushika madaraka yake.

"Jana tarehe 12 Desemba 2018 nilimwelekeza Mwanasheria Fatma Karume ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Lugango Kilangi"

Kwenye kesi hiyo, nimemwelekeza Wakili wangu kuwa Mdaiwa awe Ndugu John Pombe Magufuli na Ndugu Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aunganishwe."

Kwa vile Wakili wangu amekwishaliingiza suala hili kwenye mchakato wa kimahakama, sitaingia kwenye kiini cha kesi na badala yake nitafafaua mambo mawili; msukumo uliosababisha kesi hii kufunguliwa na mbili, sababu za kumuunganisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Joseph Pombe Magufuli.

Nitayashughulikia masuala yote mawili kwa pamoja.

Kabla ya kuyashughulikia masuala hayo kwanza tutazame usuli wa suala lenyewe.

Tangu Dk. Kilangi ateuliwe na Rais kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwezi Februari 2018, kumekuwepo na madai kwamba hayatimiza masharti ya kikatiba ya kushika nafasi hiyo.

Binafsi, kwa kutambua unyeti wa nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sikuyachukulia madai hayo kuwa porojo linalostahili kupuuzwa au habari ya kawaida inayoweza kupita bila hatua yoyote kuchukuliwa. Niliamua kufanya utafiti wa kina kujiridhisha na madai hayo.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa Mwanasheria Mkuu wa Serikali madaraka makubwa. Yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali kwenye masuala ya kisheria.

Hii ndio sababu katiba imeweka masharti maalum ya uteuzi wa mtu wa kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ibara ya 59 (2) imeweka masharti kuwa mtu anayeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu ni lazima awe mtumishi wa umma mwenye sifa za kuwa wakili kwa miaka 15 mfululizo.

Utafiti wangu umebaini kuwa Dk. Kilangi amekuwa na sifa ya kuwa wakili kwa miaka saba tuu, chini ya hata nusu ya miaka iliyowekwa na katiba. Hana pia sifa ya kuwa mtumishi wa umma kwa miaka hiyo.